Darassa: Sijaachia ‘Muziki’ kumfunika mtu - DENIS KIBINDU

Darassa: Sijaachia ‘Muziki’ kumfunika mtu

Darassa amefunguka kuwa hakuachia wimbo wa ‘Muziki’ kwa ajili ya kumfunika msanii mwingine wala wimbo wowote.
15258729_1771044743169282_1043431187525140480_n
Hivi karibuni baadhi ya mashabiki wamekuwa wakidai kuwa rapper huyo ameachia wimbo huo kwa ajili ya kufunika baadhi ya nyimbo zilizotoka hivi karibuni kwa kuwa si muda mrefu sana ameachia wimbo mpya tangu alipoachia wimbo wake wa ‘Too Much’.
Rapper huyo anayetajwa kuwa namba moja kwa sasa, amekiambia kipindi cha Friday Night Live cha EATV, “Sijatoa ‘Muziki’ ili kufunika ngoma ya mtu yoyote. Nimetoa ‘Muziki’ kama sehemu ya mipango yangu.”
Kwa sasa wimbo huo umekuwa ni kama wimbo wa taifa huku ukiwa umejiwekea rekodi yake ya kutazamwa mara milioni moja ndani ya wiki mbili.

No comments

Powered by Blogger.