Billnass adai mwaka 2016 haukuwa mzuri kwake, ‘mwaka 2017 nitafanya makubwa zaidi’
Msanii wa muziki wa hip hop, Billnass amefunguka kwa kusema kuwa
mwaka 2016 haukuwa mzuri zaidi kwake kutokana na masomo kumbana zaidi na
kushindwa kufanya muziki akiwa huru zaidi.
Rapper huyo ambaye anabukua katika chuo cha College of Business Education (CBE) jijini Dar es salaam amedai mwaka 2017 atafanya vizuri kwa kuwa ni mwaka wake wa mwisho chuo.
“Nashukuru Mungu nimefanya vizuri kwa kiasi chake lakini haukuwa mwaka mzuri kwangu kutokana na chuo kunibana, mambo yalikuwa wengi sana lakini yote ya yote mwaka unaisha na najipanga kwa mwaka ujao ambao naona nitafanya vizuri kwa sababu kwanza ni mwaka wa mwisho chuo na mwaka wa mwisho nauchukulia ni kama nimemaliza. Kwa hiyo mwaka 2017 nitafanya mambo makubwa zaidi,” alisema Billnass.
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Chafu Pozi’ ni miongoni mwa wasanii wa hip hip waliofanya vizuri ndani ya mwaka 2016 kutokana na kufanya show nyingi

No comments