Alichokizungumza Ommy Dimpoz kuhusu ugomvi wake na Diamond - DENIS KIBINDU

Alichokizungumza Ommy Dimpoz kuhusu ugomvi wake na Diamond

Kupitia kipindi cha XXL ya Cloudsfm leo Ommy Dimpoz amefunguka mengi kuhusiana kutokuwa na maelewano mazuri  na swahiba wake mkubwa na msanii mwezake Diamond Platnumz.
Haya yamekuja baada ya maneno maneno mengi ya vijembe kutokea mitandaoni kati ya wawiili hao na jana katika kipindi hicho cha XXL Diamond alisikika akisema kwamba Ommy alimtuma Salam (Meneja wa Diamond)ili wamalize tofauti zao lakini yeye alikataa na hata Omari alipojaribu kumpigia simu yeye hakupokea.

Ndipo Ommy naye alipoamua leo kuja kuelezea ya kwake kupitia hapohapo.ambapo  amesema katika urafiki wao ASsiku zote yeye ndiye alikuwa mwaminifu  zaidi katika kuudumisha urafiki wao lakini kuna wakati mwenzake alianza kuonesha kumficha baadhi ya vitu hasa vinavyohusiana na kazi.
Sikuwa tayari hata kidogo kumkosea Diamond hata siku moja ni mtu mwenye mchango mkubwa sana katika maisha yangu kimziki
lakini siku zinavyokwenda nikaona ukaribu unapungua nakumbuka baada ya msiba wa Ngwair tulienda studio nikamsikilizisha tupogo
Ni mtu pekee aleyenitia Moyo kwenye ile kazi nilimueleza kuhusu King Maluu aje kunipigia saxophone akaniambia itakuwa poa sana kesho yake sina hili wala lile nikasema nipite kwa Mako chali Daah studio namkuta D  na King Maluu>>OMMY
anasema wakiwa bado studio hapo kwa Mako chali ansema alisikia Diamond  akimuambia Mako Chali kuwa amchomee CD kwakuwa anasafiri na walipomaliza Ommy alimuuliza kuhusu safari hiyo lakini Diamond alimuambia kuwa alikuwa akimzingua tu Mako hakuna safari yoyote lakini kesho yake aliona akipost picha akiwa kwenye ndege.
nikajiuliza huyu si nilimuuliza jana kama anasafiri??si ni mwanangu,nikasema anyway labda ni safari imejitokeza ghafla you never know>>Ommy
Ndipo baadae alitonywa na rafiki yako wa karibu Halima Kimwana kuwa Diamond alienda Afrika Kusini kufanya video yake
Tukio jingine ambalo lilimuumiza  Omari ni baada ya kumuomba Diamond waende pamoja Marekani kwenye tuzo za Afrimma kwa gharama zake mwenyewe ili amsaidie kumtafutia connection lakini alidai kuwa Diamond alikuwa akimkwepa hadi alipokuja kushtuka kuwa amesafiri bila kumwambia na alipojaribu kumpigia simu kwa muda mrefu haikupokelewa hadi ilivyofika jioni ndipo Diamond alimpigia na kumwambia kuwa yuko Afrika kusini na kudai kuwa safari ilitokea ghafla
Kuhusu swala la kumtumia Wema Sepetu kwenye Video yake ya Wanjera kusemwa kwamba ni moja ya sababu ya yeye na Diamond kugombana Ommy Dimpoz amesema sio kweli yeye alimuweka wema kwasababu amekuwa na urafiki na Wema hata kabla ya kukutana na Diamond.
Hebu niambie Wema amekuwa na mahusiano na watu wangapi wengine ambao leo hii bado unaona D yuko nao close? Kwanini nilipokuwa naye mimi tu ndio imekuwa tatizo?>>Dimpoz
Kwenye ishu nyingine ambayo ilisemwa na Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram kuhusu kupumuliwa Ommy amesema Pale mtu anapotaka kukutukana hakuchagulii tusi sometime unapoitoa kauli, huwezi kujua itamwathiri mtu kwa kiasi gani, pengine itamwathiri kwa kiasi kikubwa kwasababu kuna mtu ataichukua ile kauli kiushabiki. Hata kwenye comments, mimi ninaweza kuzima comments zangu kwenye Instagram lakini nimeziacha na ukisoma comments utaona kabisa mwingine anakutukana ‘we shoga.’ Lakini as long as mimi ninajua mzima hainiathiri, kwanza hakuna tusi jipya, imeanza kutukanwa mimba>OMMY

No comments

Powered by Blogger.