Ruby Amjia Juu Said Fella - DENIS KIBINDU

Ruby Amjia Juu Said Fella

Baada ya Saidi Fella kumzulia jambo msanii Ruby ameibuka na kusema hakuwa na msongo wa mawazo wala nini ila haraka haraka zao ndizo zilisababisha asionekane kwenye video ya ngoma ya Bendi ya Yamoto.
Rubby
Rubby
Baada ya mkubwa Fella kuzungumza na eNewz na kutufahamisha kuwa mwanadada Ruby ana msongo wa mawazo, kitu ambacho kilipelekea uongozi wa Bendi ya Yamoto kufanya video bila ya dada huyo,Ruby kimemuuma sana na kusema hakuwa na msongo wa mawazo wala nini sema ni haraka haraka zao ndizo zilisababisha asionekane kwenye video hiyo.
Hata hivyo Ruby anasema wimbo huo ulirekodiwa muda mrefu sana na ulichelewa kutoka mbona hilo walivumiliana lakini kwa sasa walishindwa kumsubiri wakati yeye alijua lazima aonekane na afanyekazi yake kama ilivotakiwa.
Pia Ruby amesema amejisikia vibaya saana kuona hiyo video imefanyika bila yeye kuwepo ila yeye hajakataa kuonekana katika hiyo video kwa hiyo mashabiki zake waelewe kuwa yeye alikuwa tayari kufanya video ila upande wa Yamoto Band walikuwa na haraka na hyo video.
Ruby anasema kuwa yeye alikuwa hayupo kasafiri na walitaka afanye hiyo video wakati yeye alikuwa hayupo tayari kushuti hiyo video na wao walitaka video ifanyike haraka na yeye alikuwa busy ndio mahali walipopishana hapo na kushindwa kuwa ontime na yeye anasema, hivyo ukweni ni kwamba hana stress kabisa.
eatv.tv

No comments

Powered by Blogger.