Roma: Tutaendelea Kuichana Serikali Inapokosea - DENIS KIBINDU

Roma: Tutaendelea Kuichana Serikali Inapokosea

Msanii Roma Mkatoliki amefunguka na kusema kuwa ataendelea kuichana Serikali pale ambapo inakosea na wataisifia pale inapotenda mambo mema kwa jamii na amesisitiza kuwa yeye anaamini kuwa mpaka sasa katika uongozi wa Rais Magufuli.
ROMA 34
Roma Mkatoliki
kuna mambo mengi ya kuzungumza au ya kuimba kwani kuna matukio mengi yaliyotokea ambayo jamii inataka majibu yake.
“Tutaendelea kuichana Serikali pale inapokosea na itasifiwa pale inapofanya mambo ya msingi kwa jamii, ila mpaka sasa kuna mambo mengi ya kuimba kwenye uongozi huu, hata jamii nayo inaposikia nataka kutoa kazi watu wanaanza kujiuliza, mambo kama bunge live, Sukari, hivyo kunamambo mengi sana ya kuimba” alisisitiza Roma Mkatoliki.
Roma Mkatoliki amesema kuanzia sasa muda wowote ataachia wimbo wake mpya unaoitwa ‘Kaa Tayari’ hivyo watu wasubiri kusikia ndani ya wimbo huo ameimba nini.
eatv,tv

No comments

Powered by Blogger.