Jokate na Kiba, Mapenzi Upya! - DENIS KIBINDU

Jokate na Kiba, Mapenzi Upya!

Wapenzi mastaa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Alikiba Saleh ‘King Kiba’ wameombwa chondechonde na baadhi ya mashabiki wao kuwa sasa wafunge ndoa kwani penzi lao lina baraka ya Mungu kutokana na kukumbwa na migogoro lakini bado likaibuka kwa staili nyingine.
jokate-na-kiba
Kwa nyakati tofauti, mashabiki hao wamekuwa wakiwaombea dua njema ya kufunga ndoa kutokana na kufurahishwa na ‘kapo’ (couple) yao kwani kila mmoja anaendana na mwenzake.
Wiki mbili zilizopita mashabiki walianza kuwaombea dua na kuwatupia maoni kupitia mitandao ya kijamii wakiwataka kufunga ndoa baada ya kuona picha zao wakiwa pamoja kwenye hafla ya kufuturu huku kukiwa na minong’ono kuwa penzi lao bado lipo na sasa lipo siriasi.
“Hivi mmewaona Jojo (Jokate) na Kiba wanavyopendezana? Jokate mwezi huu anavaa mavazi ya Kiislam ili kuhakikisha anakwenda sambamba na imani ya ‘mista’ wake (Kiba).
“Hata hivyo, nasikia Kiba amemkataza Kidoti kuongea na vyombo vya habari lakini penzi lao bado lipo palepale,” alinyetisha mmoja wa mashabiki hao ambaye ni rafiki wa karibu wa mastaa hao.
Rafiki huyo alikwenda mbele zaidi na kudai kuwa, kuna wakati Jokate alikuwa akiumwa malaria, wifi yake, Zabibu (dada wa Kiba) alikwenda kumuona nyumbani kwake (Oysterbay, Dar) na kumpelekea dawa, hali inayoonesha bado kuna uelewano mzuri na familia yao.
“Kama huamini kaangalie kwenye ukurasa wake (Jokate) wa Instagram, kuna siku alimshukuru Zabibu kwa kumhudumia na mara ya mwisho aliposti mpaka picha ya mtoto wa Kiba siku yake ya kuzaliwa. Kwa mtu ambaye yuko naye mbali hawezi kuwa huru hivyo,” alisema sosi huyo.
Sosi huyo alisema kuwa, sasa hivi Kiba hawezi kumuongelea vibaya Jokate kwani kuna kipindi alihojiwa kwenye televisheni moja na kummwagia sifa kibao huku akimuombea kupata mwanaume ambaye hatamuumiza.
“Nadhani kipindi mlikiona, Kiba anavyomsifia Jokate, kwa kawaida tu ukiona kipindi kile utaelewa tu kuwa ni wapenzi, tuwaombee ndoa tu kwani wanapendezana na hakuna anayeweza kumsema mwenzake vibaya,” alisema sosi huyo.
Baada ya kumwagiwa ishu hiyo, mwandishi wetu alimtafuta Kiba bila mafanikio lakini akampata Jokate kwa njia ya simu na kumsomea mashtaka yake kuwa anakatazwa na Kiba kuongea na vyombo vya habari lakini mashabiki wanawaomba wafunge ndoa ambapo alishangaa na kukaa kimya kisha akajibu: “Mnapenda sana tetesi walahi.” Kisha akaingia mitini na hata alipotumiwa chatting kwenye WhatsApp hakujibu.
Kisanaa, hivi karibuni, Jokate ambaye ni mwigizaji, mtangazaji na modo, alionekana kwenye uandaaji wa Video ya Mboga Saba ya Herry Samir ‘Mr Blue’ ambayo amemshirikisha Kiba na wote wakionekana wenye furaha tofauti na wapenzi waliogombana ambao huwa ni nadra kushiriki kitu cha pamoja.
Jokate na Kiba mara ya mwisho waliripotiwa kuwa wameachana na kwamba jamaa huyo amepata mrithi wa Jokate kutokana na penzi lao kuzimika na kufufuka.
Chanzo:GPL

No comments

Powered by Blogger.