Fanya hivi ili kuweka bold na italic kwenye WhatsApp
WATU wengi husumbuka sana wanapoandika ujumbe kwenye mtandao wa WhatsApp kutokana na hali kwamba herufi huwa na uzito sawa wa rangi katika hali ya kawaida, aidha, mtindo wake huwa mmoja.
Je, wajua unaweza kukoleza rangi ya herufi na kuzifanya nzito (bold), ukaziweka kwa mlazo (italiki) na pia ukaweka mstari unaozikata herufi kati, kwa Kiingereza strikethrough?
Unachohitaji kufanya kwanza kabisa ni kuwa na toleo la karibuni zaidi la app ya WhatsApp kwenye simu yako.
Kuweka bold
Ili kukoza rangi kwenye herufi (kufanya bold), unahitajika kutanguliza neno lako na alama ya nyota na kisha kuhitimisha na alama ya hiyo hiyo nyota.
Kwa mfano, ukiandika *bold* itatokea ikiwa bold
Kuweka italiki
Ili kufanya herufi zako kuwa za mlazo au kuwa za italiki, unahitajika kutanguliza na mstari sakafu (underscore) na kuhitimisha na alama iyo hiyo.
Ukiandika _italics_ itatokea ikiwa italics
Kuweka strikethrough
Ukitaka kuweka alama ya kukata kati kwenye herufi zako, unahitajika kuanza na alama ya mawimbi au kwa Kiingereza tilde (~) na kuhitimisha na alama iyo hiyo.
Ukiandika ~strikethrough~ itatokea ikiwa na mstari uliokata herufi kati.
uunganisha mitindo
Unaweza ukataka kuunganisha mitindo, mfano utake kuwa na bold na italiki.
Utahitajika kutumia alama za unachohitaji katika kuanza neno lako na kuhitimisha.
Mfano, ukiandika _*bolditalics*_ inafaa kutokea ikiwa bolditalics.
No comments