Belle 9 kuchangia asilimia 10 ya mapato ya BMS Tour kusaidia wazee wa kituo cha Funga Funga Moro - DENIS KIBINDU

Belle 9 kuchangia asilimia 10 ya mapato ya BMS Tour kusaidia wazee wa kituo cha Funga Funga Moro

Belle 9 anatarajia kutoa asilimia 10 ya mapato atakayoingiza kwenye show yake ziara ya BMS mjini Morogoro kusaidia kituo cha kulelea wazee wasiojiweza cha Funga Funga kilichopo mkoani humo.
2f39ece5-390d-4403-b982-d407fa417a47
Belle amekusanya wasanii kibao kumsindikiza kwenye ziara yake ya BMS mjini Morogoro siku ya Eid Pili.
Wasanii watakaomsindikiza ni pamoja na Jay Moe, Izzo Bizness, Afande Sele, Shilole, Mo Music, O-Ten, Dayna Nyange, Stamina, Darassa na wengine.
Mshereheshaji kwenye show atakuwa mtangazaji wa Clouds FM, B12.
Wiki iliyopita alikitembelea kituo hicho na kutumbuiza mbele ya wazee hao.

No comments

Powered by Blogger.