Barakah Da Prince adai hajawahi kuupenda muziki wa Young Killer - DENIS KIBINDU

Barakah Da Prince adai hajawahi kuupenda muziki wa Young Killer

Msanii wa muziki, Barakah Da Prince, amefunguka na kusema kuwa yeye si shabiki na wala hapendi muziki anaoufanya rapa na mzaliwa mwenzie wa Mwanza Young Killer Msodoki.
Barakah Da Prince
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Siwezi’ ameiambia Times Fm, kuwa hapendi muziki wala hajawahi kupenda kazi yoyote ya Msodoki.
“Sijawahi kupenda muziki anaoufanya Killer,” alisema Barakah. “Mi sio shabiki yake kabisa, najua ndio anatokea home na nini lakini sipendi muziki wake,”
Katika hatua nyingine amesema rapa anayemkubali zaidi ni Young Dee kwa kuwa anauwezo wa kubadilika kulingana na Mazingira

No comments

Powered by Blogger.