AY asema Crazy GK ana ngoma kali itayoifunika ‘Hii Leo’ - DENIS KIBINDU

AY asema Crazy GK ana ngoma kali itayoifunika ‘Hii Leo’


Msanii mkongwe wa muziki, Ambwene Yessayah ‘AY’ amefunguka kwa kusema kuwa msanii mwezake wa kundi la East Coast Team, Crazy GK ana ngoma kali ambayo itakuja kuufunika wimbo wake wa zamani uitwao ‘Hii Leo’ ambao alishirikishwa yeye pamoja na Mwana FA.
page10
Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na Zigo remix, amekiambia kipindi cha TheBase cha ITV kuwa ngoma hiyo pia ameshirikishwa yeye pamoja na Mwana FA.
“GK tumesharekodi tayari ana bonge la ngoma, ana bonge la ngoma, ngoma ambayo inaweza ikafukia ‘Hii Leo’,” alisema AY. “Ni kweli kabisa ninachosema, na nimefanya mimi GK na Mwana FA,”
Aliongeza, “Leo ninaweza kuwa ni msemaji wake, ngoma ipo tayari tunataka kufanya video alafu atapanga ataachia lini hiyo ngoma, lakini ni ngoma kubwa. Kwa mwaka 2016 wimbo wa rap mkali sijausikia,”
AY alisema bado hajajua ni lini rapper huyo ataamua kuachia wimbo huyo baada ya kukamilika video yake.

No comments

Powered by Blogger.