Isikupite Hii Mpya Kutoka Kwa Jux Na Vanessa Mdee
Tukiongelea Couple zenye ushawishi na idadi kubwa ya mashabiki hatuwezi tukaacha kuwataja Vanessa Mdee na African Boy Jux,
Licha ya wote kuwa kwenye Industry moja (Muziki) lakini wawili hawa hawakuwahi kufanya ngoma ya pamoja ukiachia mbali kolabo zilizowakutanisha kama Safari ya Nikki Wa Pili na Monifere ya Gosby..
Goodnews kutoka kwa Couple hiyo ni ujio wa Colabo yao iliyopewa jina “JUU” ambayo Producer Lupa amehusika.
Wawili hao wameshare kava la ngoma hiyo iliyotayarishwa na Lufa katika studio za Switch Records. “Kuna muda mi nashindwa kufanya vitu vingi kwako natamani kutimiza #Juu,” ameandika Vanessa kwenye Instagram katika picha ya kava hilo.
“Ila moyo unajua jinsi gani navyotaka kwenda sawa na wewe #Juu,” ameandika kwenye nyingine.
Naye Jux ameandika: Upendo wetu ndo muhimu kuwa pamoja mimi na wewe usije nipa wazimu kisa nakupenda we #JUU.”
Huo unakuwa wimbo wao wa kwanza kuutoka rasmi tangu wawe pamoja.
No comments