Ripoti: Wizkid kuungana na Davido Sony Music Worldwide - DENIS KIBINDU

Ripoti: Wizkid kuungana na Davido Sony Music Worldwide

Wizkid yuko mbioni kutangazwa msanii mpya wa Sony Music Worldwide, kwa mujibu wa kituo cha runinga cha Soundcity.
13696965_1248290765189225_969618485_n
Kituo hicho kimeripoti kuwa muimbaji huyo ataungana na Davido kwenye roaster ya label hiyo kubwa.
“Dili la Wizkid na Sony limekamilika. Habari itatoka hivi karibuni. Meneja wake Sunday Are ametuelezea kuwa hili litazungumzwa hivi karibuni,” kilisema chanzo.
Umaarufu wa Wizkid umeongezeka maradafu mwaka huu baada ya kushirikishwa na Drake kwenye wimbo One Dance ulioshika namba moja kwenye chati za Billboard Hot 100.
Jumamosi iliyopita staa huyo alitumbuiza jijini Mwanza kwenye Fiesta.

No comments

Powered by Blogger.