Belle 9: Kwanini wabongo hatutaki kukubali Diamond ni msanii mkubwa Afrika?
Belle 9 amekana kusaini na WCB na kudai kuwa alienda kutembelea
kwenye ofisi zao kwakuwa Diamond ni msanii mkubwa Afrika na amefanikiwa
kufika mbali kimuziki.
“Diamond ni msanii mkubwa Afrika ila Watanzania tumekuwa wagumu
kulikubali hilo,” amekiambia kipindi cha E News cha EATV. Belle 9
aliongeza kuwa alienda WCB kwa ajili ya kuwatembelea na kufanya nao
mazoezi kwa sababu anamheshimu Babutale kwakuwa ndiye aliyemkutanisha na
menejimenti yake aliyonayo.
Katika hatua nyingine, muimbaji huyo amesema kuwa bado ana mkataba na menejimenti yake hivyo hawezi kusaini mkataba kwingine labda mpaka utakapomalizika. Na kuhusu WCB amesema anaweza akasaini nao endapo wakikubaliana na mambo yakienda sawa.
Hata kwa Rich Mavoko ilikuwa ni sinemaa kama hii lakini hatimaye alijiunga na familia ya Wasafi.

No comments