Wasanii Hawa Kunogesha ZIFF Mwaka Huu - DENIS KIBINDU

Wasanii Hawa Kunogesha ZIFF Mwaka Huu

WASANII wa hip hop, Farid Kubanda ‘Fid Q’, Juma Kassim ‘Juma Nature’, Stamina na Young Killer ni miongoni mwa wasanii watakaonogesha Tamasha la 19 la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi maarufu ZIFF, linalotarajiwa kuanza maonyesho yake Julai 9 hadi 17 visiwani Zanzibar.
NYALUSI
Daniel Nyalusi
Tamasha hilo limezinduliwa rasmi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki likiwa na kauli mbiu ya ‘Ndiyo hii Safari Yetu’.
Meneja wa Tamasha hilo, Daniel Nyalusi, alisema kwa mwaka huu tamasha hilo limeshirikisha
vyombo mbalimbali vya fi lamu vikiwemo Nollywood, Bollywood na Hollywood ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Kunal Kapoor kutoka nchini India.
“Kuna wasanii wengi tumewashirikisha lakini kuna mmoja kutoka Marekani tumemfanya
‘surprise’ hivi karibuni tutamuweka wazi lakini pia tumepokea filamu 490 kutoka nchi 32 na filamu 80 zimepitishwa, fi lamu za Bongo ni 15.
Mtanzania

No comments

Powered by Blogger.