Video,Muonekani wa studio mpya ya WCB Wasafi, Picha ya Ali Kiba ukutani
Meneja wa Diamond, Babu Tale ameonyesha kuwa wao hawana tatizo na
Alikiba baada ya kupost kipande cha video kinachoonyesha picha ya msanii
huyo ndani ya studio ya Wasafi Records
Ni muda mrefu imezungumzwa kuwa Diamond na Alikiba wana bifu mpaka
kupelekea kuanzishwa kwa baadhi ya team za mitandaoni za kukejeli
mafanikio ya msanii wa team nyingine lakini hiyo ni dalili kuwa ipo siku
itabaki historia tu.Babu Tale alipost kipande hicho cha video kinachoonyesha baadhi ya picha za wasanii wakubwa Bongo akiwemo Marehemu Bi Kidude, Mr Blue, Dully Sykes, Juma Nature, Q Chief, Alikiba na wengine wengi.
Je, hiyo inaweza ikawa ndiyo kiki ya kuikaribisha video ya wimbo mpya wa Diamond aliowashirikisha P Square ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni?
Tazama video hapa.
No comments