Ni headline baada ya headlines… Navy Kenzo wapata shavu jipya
Ni Headlines za kundi la Navy Kenzo linaloundwa na Nahreel na Aika limechaguliwa kuwa mabalozi wapya wa Application ya simu iitwayo Klobaa inayohusika kuwakutanisha watumiaji wa hiyo application hiyo sehemu mbalimbali za burudani nyakati za usiku kama Clubs na Lounges pamoja na matukio mbalimbali.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Aika alisema…’Hawa
wamekuwa wakitutafuta tangu mwaka 2015 hili shavu tulikuwa tunazungumza
nao kwahiyo mwisho wa siku tukakubaliana na tukapewa ubalozi kwahiyo
watakuwa wakitutumia sisi kama kutangaza Application yao, tumesaini nao
mkataba wa miaka miwili‘- Aika
‘Kazi yangu sisi ni kusafiri nao wanatuonyesha jinsi ya watu wanavyostarehe
katika Clubs, Lounges pia kutangaza kazi zetu za muziki kupitia shavu
hili tutaenda nao Marekani, Dubai, South Africa na nchi nyingine
kuitangaza hii Application yao mpya tukiwa na kazi zetu– Aika
No comments