Alikiba na Lady Jaydee kuachia album zao mwaka huu - DENIS KIBINDU

Alikiba na Lady Jaydee kuachia album zao mwaka huu

Alikiba na Lady Jaydee wataachia album zao (kila mmoja na yake), mwaka huu, kwa mujibu wa meneja wao, Seven Mosha.
Seven
“Wote watadrop album zao mwaka huu,” Seven alimweleza mtangazaji wa kipindi cha Super Mega cha Kings FM, Divine Kweka.
“Baada ya kutoa album kila mmoja atakuwa na international collaboration na nyimbo zingine ambazo hazijatoka, kabla ya album zao kutoka mwezi wa 11. Kila mmoja na album yake, haitokuwa tarehe moja lakini ni kwenye mwezi wa 11. Lakini kabla mwaka haujaisha wote watadrop album zao,” aliongeza Seven.
Seven amekiri kuwa utoaji wa album wa kawaida (traditional ) umeanza kufifia duniani kote na kwamba sasa hivi mfumo wa kidijitali umekuwa na nguvu hivyo ni njia watakayoitumia zaidi.
“Kwahiyo kama distribution yako kama ni nzuri kama wakati huu Alikiba distribution rights amesaini na Sony muziki wake ukitoka kama tulitangaza juzi juzi nyimbo yake kama Aje inapatikana stores 750 kila sehemu, kwahiyo kama una distribution channel nzuri kama hiyo hapo then album inaweza kutoka,” amesisitiza.
Amedai pia kuwa Lady Jaydee naye atakuwa na mfumo kama huo wa usambazaji.
Msikilize zaidi hapo chini.

No comments

Powered by Blogger.