AliKiba aanza kushoot video ya ‘Aje remix’ akiwa na M.I - DENIS KIBINDU

AliKiba aanza kushoot video ya ‘Aje remix’ akiwa na M.I

Mkali wa wimbo ‘Aje’ AliKiba baada ya kufanya vizuri na original version ya wimbo huo, ameweka kambi nchini Afrika Kusini kuandaa remix ya wimbo huo akiwa amemshirikisha msanii wa Nigeria, M.I.
KOROGA-FESTIVAL-PRESS-CON-ALIKIBA-NAIROBI-NOV-2015-5-1024x683
Awali kolabo hiyo ya ‘Aje’ akiwa na M.I ilivuja katika mitandao ya kijamii wakati haijamalizika hali ambayo ilimfanya kuachia original version yake.
Kwa mujibu wa video ya AliKiba iliyozagaa katika mitandao ya kijamii, inamuonyesha muimbaji huyo akiwa location Africa Kusini huku akizungumza project hiyo.
“Tunashoot video, ‘Aje remix’ video nikuwa na M.I,” alisema AliKiba.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa yupo Afrika Kusini, amedaiwa kushoot video mbili mpaka sasa, moja ya kolabo yake na Barakah The Prince na nyingine ya kolabo yake na M.I.

No comments

Powered by Blogger.