Shilole Kutafuta Mume Kijijini
MKALI wa Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amejutia
kuwapenda wanaume wa mjini kuwa ni wavivu kila sekta hivyo anajipanga
kwenda kijijini kwao Igunga,Tabora kutafuta mume.
Akistorisha na Showbiz Xtra, Shilole alisema kuwa, hataki tena
kujichosha akili kwa wanaume wa mjini kwa vile ni wavivu bora aende
Igunga kumpata mwanaume atakayeweza kufanya kazi kutokana na vyakula
asili anavyokula.
“Wanaume wa mjini wamezoea chipsi mayai, hawawezi chochote bora wa
kijijini wanakula dona na wana akili za kufikiria,” alisema Shilole.
Shilole alikuwa akitoka kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda
No comments