Lollypop akanusha kuandika Ibaki Story ya Rich Mavoko
Producer, mwandishi wa nyimbo za Bongo Flava na muimbaji wa nyimbo za injili, Goodluck Gozbert ama kama anavyojulikana pia kama Lollypop, amekanusha kuandika wimbo wa Rich Mavoko, Ibaki Story.
Tetesi hizo zimekuwepo wiki hii na Rich tayari amezungumzia na kudai kuwa kuna vitu kadhaa Lollypop aliweka kwenye wimbo huo lakini si kwamba aliandika.
Akiongea na kipindi cha Super Mega cha Kings FM kinachoendeshwa na Divine Kweka, muimbaji huyo alisema:
"Mavoko tunafahamiana na tumewahi kuonana mara chache lakini
kuhusu hiki kinachoendelea kutrend kwakweli sifahamu na tumewasiliana
pia kuhusu hili akaniambia anashangaa, nikamuambia mimi pia nashangaa
kuhusu hilo kwahiyo ni kitu ambacho sielewi kimetokana na nini na ni
kwanini kinazungumzwa
No comments