Huu ni uthibitisho kutoka kwa Babu Tale kuwa Chidy Benz kajiunga Rasmi WCB
Inawezekana sana kuwa Chidi Benz amejiunga rasmi na lebo ya WCB, hii inatokana na Meneja wa Babu Tale kuandika Maneno yanayothibitisha kuwa Chidy Benzi sasa yuko kwenye himaya hii yenye nguvu katika Muziki wa Tanzania.
Chidy Benz akiwa na Babu Tale
Katika Mtandao wa Instagram kupitia account ya Babu Tale mwenyewe ameandika "Mahindi Yameota Kwenye Shamba La Kibogoyo..!! @officialchidibeenz #newchidibeenz"....
Pia katika account mpya ya Instagram inayomilikiwa na Chidy Benz mwenyewe, amepost picha akiwa na Harmonize na kuandika "Nipo na mdogo wangu @harmonize_tz #NewChidiBeenz #TheReturnOfKingKong #Chuma."
Chidy Benz akiwa na Harmonize
No comments