Hii ni orodha nzima ya wasanii watakaotumbuiza kwenye BET Awards June 26
Future, Usher, na
Bryson Tiller wametangazwa kuongezwa kwenye orodha ya wasanii
watakaotumbuiza siku hiyo. Wanaungana na mastaa wengine waliokuwa
wametangazwa awali ambao ni pamoja na Alicia Keys, Maxwell, pamoja na
tribute ya Prince itakayotolewa na D’Angelo, The Roots na Janelle MonĂ¡e.
Mastaa
watakaokabidhi tuzo ni pamoja na DJ Khaled, Gabrielle Union, Tinashe,
Fantasia, Regina Hall, Birdman, Jermaine Dupri, Dame Dash na Snoop Dogg.
Diamond ni miongoni mwa wasanii wanaowania tuzo hizo mwaka huu kwenye kipengele cha Best International Act: Africa.
Washereheshaji wa show hiyo watakuwa ni Anthony Anderson na Tracee Ellis Ross.
Tuzo hizo zitatolewa June 26 live kutoka Microsoft Theater, Los Angeles, Marekani.
No comments