Dawa za Kulevya Kwangu Itabaki Historia- Chid Benz - DENIS KIBINDU

Dawa za Kulevya Kwangu Itabaki Historia- Chid Benz

Mkali katika muziki wa Bongo Fleva, Rashidi Makwiro ‘Chid Benz’, amesema matumizi ya dawa za kulevya yamempa mafunzo makubwa na itabaki kuwa historia kwake.
chid
Chid Benz aliliambia MTANZANIA kwamba dawa za kulevya zimeharibu maisha yake kwa kiasi kikubwa na yamemdhalilisha yeye na familia yake na watu wake wa karibu hivyo hatathubutu kurudia kama baadhi ya wasanii walioacha na kurudia kama Rehema Chalamila ‘Ray C’.
“Dawa za kulevya kwangu zinabaki kuwa historia, sitaki hata kuzisikia zimeniumiza sana kimawazo, zimenidhalilisha na zimepoteza mwelekeo wa maisha yangu, sina hamu nazo tena nina hasira nazo siwezi kuzirudia kama baadhi ya wengine walivyorudia kwa sasa naangalia maisha yangu mapya katika muziki,” alijieleza Chid Benz.
Chid Benz anaeleza kwamba waliomshawishi kuingia katika matumizi ya dawa hizo ni marafiki zake katika makundi aliyokuwa akibadilishana nao mawazo ambao wengi wao walimshawishi kwamba akitumia dawa hizo atakuwa na nguvu zaidi ya kuimba na kufanya makubwa jukwaani lakini ikawa tofauti na matarajio.

No comments

Powered by Blogger.