Babu Tale kayaongea haya kuhusu Diamond Platnmuz na Alikiba
‘Kwanza watu wanatakiwa kufahamu kuwa pale sisi tulialikwa kwa ajili ya futari na tulipofika pale wenyeji wetu walituomba sisi kama celebrity kupiga picha ya pamoja na ndio ile picha ambayo tumepiga mimi Alikiba, Ommy Dimpoz na wengine nataka ifahamike kuwa mimi sina tofauti na Alikiba wala Diamond hana tofauti yeyote ile na Alikiba‘>>>Babu Tale
‘Alafu kingine ambacho watu hawakifahamu ni kuwa mwaka jana Diamond na Alikiba walikutana studio na hadi picha walipiga, video pamojana sauti zao pia zipo na hivi karibuni nitaipost ile picha ili kuwaonyesha watu hakuna tatizo ni biashara tu>>>Babu Tale
No comments